Hassan Eslayeh, mpiga picha huru aliyeheshimiwa sana, alikuwa akipokea matibabu katika Hospitali ya Nasser mjini Khan Yunis, kusini mwa Ukanda wa Gaza, siku ya Jumanne, baada ya kunusurika katika shambulio la anga la Israel tarehe 7 Aprili lililolenga hema la wanahabari.
Eslayeh alikuwa akifuatilia na kuripoti vita vya mauaji ya kimbari vinavyoendelezwa na Israel dhidi ya Gaza tangu Oktoba 2023, pamoja na oparesheni ya kihistoria iliyoendeshwa na Hamas na wapiganaji wengine wa upinzani kutoka Gaza dhidi ya maeneo ya Palestina yaliyokaliwa kwa nguvu, kabla ya kuzuka kwa vita hivyo.
Mwandishi huyo alikuwa na wafuasi wengi katika mitandao ya kijamii, akijulikana kwa uandishi wake wa ukweli usioficha hali halisi ya mashambulizi dhidi ya raia.
Jeshi la Israel lilidai kuhusika na shambulio hilo la anga lililosababisha kifo chake, likidai kuwa walikuwa wakilenga “kituo cha uongozi na udhibiti” cha Hamas ndani ya hospitali hiyo. Hata hivyo, kauli hiyo inafuatia msururu wa mashambulizi mengine ya vifo vingi vya raia ambayo Israel mara nyingi huwapatia maelezo kama hayo.
Hamas pamoja na wachambuzi huru wamekanusha madai hayo, wakisisitiza kuwa Eslayeh alikuwa mwanahabari raia asiye na uhusiano wowote na vikundi vya Muqawama vya kijeshi.
Vuguvugu hilo la Muqawama lilitaja shambulio hilo kama “ukiukwaji wa wazi wa sheria zote za kimataifa na za kibinadamu,” na kusema kuwa utawala wa Israel umeporomoka kimaadili na kihabari.
Hamas pia imetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa, ikiwemo Umoja wa Mataifa na mashirika ya wanahabari, kuchukua hatua za haraka kusitisha uhalifu wa kivita wa Israel dhidi ya waandishi wa habari wa Kipalestina na kuiwekea vikwazo serikali ya Tel Aviv.
Tangu kuzuka kwa vita hivyo, waandishi wa habari wa Kipalestina zaidi ya 215 wameripotiwa kuuawa na majeshi ya Israel, wengi wao wakiwa Gaza.
Zaidi ya Wapalestina 52,800 wameuawa Gaza katika vita vya mauaji ya kimbari ambavyo utawala wa Kizayuni wa Israel ulianzisha Oktoba 2023, wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto.
Your Comment